Miongoni mwa Aina za Tabligh ni: Tablighi ya vitendo (tabia na mwenendo): Kwa maana: Kuonyesha maadili ya Kiislamu kwa matendo mema na mfano mwema.

20 Desemba 2025 - 19:34

Malawi | Darsa ya Maadili yafanyika katika Madrasa ya Al-Hadi (as)

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt as -ABNA- Madrasa ya Al-Hadi (as) Nchini Malawi imefanya Darsa ya Maadili katika eneo la musala ya Madrasa hiyo, kuanzia saa 2:00 hadi 3:00 baada ya adhuhuri. Darsa hiyo imeendeshwa na Sheikh Abdul Rashid Yusuf, kwa kushirikisha wanafunzi ya elimu ya dini wa Madrasa hiyo ya Kiislamu.

Malawi | Darsa ya Maadili yafanyika katika Madrasa ya Al-Hadi (as)


Mada ya darsa la Maadili : Tablighi (Ulinganiaji)
Katika darsa hiyo, Sheikh Abdul Rashid Yusuf amefafanua maana ya tablighi akieleza kuwa, kwa upande wa lugha, tablighi ni kufikisha, kuwasilisha na kupeleka ujumbe. Kwa upande wa istilahi ya kidini, tablighi ni kuwafikishia watu ujumbe wa dini, hukumu za Mwenyezi Mungu, maadili mema na maarifa ya Kiislamu kwa njia sahihi na yenye hekima.
Aidha, darsa imeelezea aina mbalimbali za tablighi, zikiwemo:
1_Tablighi ya maneno (ya kusema):
Kama vile hotuba, khutba, nasaha na ufundishaji; hii ni miongoni mwa njia zilizoenea zaidi katika ulinganiaji.
2_Tablighi ya vitendo (tabia na mwenendo):
Kuonyesha maadili ya Kiislamu kwa matendo mema na mfano mwema.
3_Tablighi ya maandishi:
Kupitia vitabu, makala, vipeperushi na maandishi mbalimbali yenye kuelimisha.
4_Tablighi ya mtu binafsi na ya kijamii:
Ulinganiaji unaofanyika kwa mtu mmoja mmoja au kwa jamii kwa ujumla.
Washiriki wamepongeza darsa hiyo kwa kuwa imeongeza uelewa juu ya wajibu wa tablighi na umuhimu wake katika kueneza maadili mema na mafundisho sahihi ya Uislamu katika jamii.

Malawi | Darsa ya Maadili yafanyika katika Madrasa ya Al-Hadi (as)

Your Comment

You are replying to: .
captcha